in , , , , , , , ,

HESLB Majina Ya Waliopata Mkopo Awamu Ya Nne 2024/2025

HESLB Majina Ya Mkopo Awamu Ya Kwanza 2024/2025 Academic Year
HESLB
ORODHA YA NNE YA WANUFAIKA WA MKOPO HESLB 2024/2025 YATANGAZWA

💥💥UNASUBIRI NINI? FOLLOW US ON INSTAGRAM. CLICK HERE!💥

HESLB YATANGAZA ORODHA YA NNE WANUFAIKA 2024/2025

HESLB,
Majina Ya Waliopata Mkopo Awamu Ya Nne 2024/2025 Academic Year, Majina
Ya Waliopata Mkopo 2024/2025, Majina Ya Waliopata Mkopo Awamu Ya Nne
2024/2025, Majina Ya Waliopata Mkopo Awamu Ya Nne 2024, Waliopata Mkopo
Awamu Ya Nne 2024/2025, Waliopata Mkopo Awamu Ya Nne 2024, Majina ya
Mkopo Awamu Ya Nne 2024/2025, Wanuafaika wa Mkopo HESLB 2024/2025.

HESLB Majina Ya Mkopo Awamu Ya Nne 2024/2025 Academic Year

9,068 WAPANGIWA MIKOPO YA TZS 27.5 BILIONI AWAMU YA NNE

Dirisha la Rufaa kufunguliwa Novemba 4 -11, 2024

Bodi ya Mikopo ya
Wanafunzi wa Elimu ya Juu leo (Jumanne, Oktoba 29, 2024) imetangaza
Awamu ya Nne (Batch Four) yenye wanafunzi 9,068 wa shahada ya awali
(Bachelor Degrees) na stashahda (Diploma) waliopangiwa mikopo yenye
thamani TZS 27.52 bilioni kwa mwaka wa masomo 2024/2025.

Wanafunzi
4,400 wa mwaka wa kwanza waliodahiliwa katika taasisi mbalimbali za
elimu ya juu zilizopo nchini kwa ajili ya masomo ya shahada za awali na
wamepangiwa mikopo yenye thamani ya TZS 13.74 bilioni. Awamu hii pia
imewajumuisha wanafunzi 2,646 wa shahada ya awali wanaoendelea na masomo
ambao wamepangiwa mikopo kwa mara ya kwanza (first-time continuing)
yenye thamani ya TZS 8.37 bilioni.
Read Also:

Mikopo kwa Stashahada

Katika
awamu ya nne iliyotangazwa leo, wamo pia wanafunzi wapya 2,022 wa
stashahada wa mwaka wa kwanza ambao wamepangiwa mikopo yenye thamani ya
TZS 5.41 bilioni. Wanafunzi hawa wamedahiliwa katika programu za
kipaumbele katika vyuo mbalimbali vya kati hapa nchini.

Ruzuku ya ‘Samia Scholarship’
Mpaka
sasa, jumla ya TZS 3.14 bilioni zimetolewa kwa ajili ya ruzuku kwa
wanafunzi 625; (588 awamu ya kwanza, 11 awamu ya pili na 26 awamu ya
tatu) kwa wanafunzi wa shahada ya awali, mwaka wa kwanza wanaonufaika na
‘Samia Scholarship’ kwa mwaka wa masomo 2024/2025 katika fani za
Sayansi, Teknolojia, Uhandisi, Hisabati na Tiba.

Kufunguliwa kwa Dirisha la Rufaa 2024/2025

Kupitia
taarifa hii, wanafunzi walioomba mikopo kwa mwaka wa masomo 2024/2025
lakini hawakuridhika na viwango vya awali walivyopangiwa au
hawajapangiwa mikopo, wanashauriwa kukata rufaa ndani ya siku saba
kuanzia Jumatatu, Novemba 4 hadi Jumapili, Novemba 10, 2024.

Imetolewa na:
Mkurugenzi Mtendaji,
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu,
DAR ES SALAAM.

KUCHEKI MAJINA HESLB, CLICK HERE!

logoblog





JOIN US ON TELEGRAM
Get Notifications Faster by:

Monitoring & Evaluation Assistant at Amref Tanzania

144 New FORM FOUR and Above Government Jobs at TEMESA – Various Posts