in , , , , , , , ,

Majina Ya Waliopata Mkopo HESLB Awamu Ya Pili 2024-2025

HESLB Majina Ya Mkopo Awamu Ya Kwanza 2024/2025 Academic Year
HESLB
ORODHA YA PILI YA WANUFAIKA WA MKOPO HESLB 2024/2025 YATANGAZWA

💥💥UNASUBIRI NINI? FOLLOW US ON INSTAGRAM. CLICK HERE!💥

HESLB YATANGAZA ORODHA YA PILI WANUFAIKA 2024/2025

HESLB,
Majina Ya Waliopata Mkopo Awamu Ya Pili 2024/2025 Academic Year, Majina
Ya Waliopata Mkopo 2024/2025, Majina Ya Waliopata Mkopo Awamu Ya Pili
2024/2025, Majina Ya Waliopata Mkopo Awamu Ya Pili 2024, Waliopata Mkopo
Awamu Ya Pili 2024/2025, Waliopata Mkopo Awamu Ya Pili 2024, Majina ya
Mkopo Awamu Ya Pili 2024/2025, Wanuafaika wa Mkopo HESLB 2024/2025.

HESLB Majina Ya Mkopo Awamu Ya Pili 2024/2025 Academic Year

Wanafunzi wa shahada mwaka wa kwanza 30,311

Wanufaika 2,157 mikopo ya ‘Diploma’

Wanafunzi 588 kunufaika na ‘Samia Scholarship’

TZS 99.7 bilioni kutumika kuwagharimia mikopo, ruzuku TZS 2.9 bilioni

Bodi
ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) leo Jumatano (Oktoba 09,
2024) imetangaza awamu ya pili ya orodha ya wanafunzi wenye sifa
waliopangiwa mikopo na ruzuku kwa ajili ya mwaka wa masomo 2024/2025.

Makundi ya walionufaika katika Awamu ya Pili

Orodha
iliyotangazwa leo inajumuisha wanafunzi wa mwaka wa kwanza
waliodahiliwa katika vyuo mbalimbali vya elimu ya juu na vyuo vya kati
waliopangiwa mikopo kwa ajili ya Shahada ya awali (30,311) yenye thamani
ya TZS 93.7 bilioni. Orodha ya awamu ya pili inafanya idadi ya jumla ya
wanafunzi 51,645 waliopangiwa mikopo katika awamu ya kwanza na awamu ya
pili kwa ajili ya kugharimia masomo yao ya shahada ya awali ikiwa na
thamani ya TZS 163.8 bilioni. Kati ya wanafunzi hao, wanafunzi wa kike
ni 22,216 (sawa na 43%) na wa kiume 29,429 (sawa na 57%)

Awamu
hii ya pii inajumuisha pia mikopo ya Stashahada (Diploma) kwa wanafunzi
wapatao 2,157 yenye thamani ya TZS 5.6 bilioni. Wanafunzi wengine 45 ni
wa shahada ya uzamili waliopangiwa mikopo yenye thamani ya TZS 205.6
milioni na wanufaika 16 wa Shahada ya Uzamivu waliopangiwa mikopo yenye
thamani ya TZS 215.6 milioni.

Kuhusu kutangazwa kwa orodha ya Awamu ya Tatu

HESLB
inaendelea kupokea taarifa za udahili kuwezesha kupanga mikopo na
kutangaza Awamu ya tatu ya orodha ya wanafunzi waliopangiwa mikopo kwa
mwaka 2024/2025 itakayotangazwa siku chache zijazo ili kuwawezesha
wanafunzi waliopangiwa mikopo kuendelea na taratibu za kujisajii katika
vyuo walikodahiliwa.
Read Also:

Samia Scholarship

Taarifa
hii pia ina idadi ya wanafunzi 588 wa shahada ya awali watakaonufaika
na fursa za ‘Samia Scholarships’ kwa mwaka huu 2024/2025, ambao
wamepangiwa ruzuku yenye thamani ya TZS 2.9 bilioni. Wanafunzi hawa ni
wenye ufaulu wa juu katika tahasusi za sayansi na waliodahiliwa katika
vyuo mbalimbali kwenye fani za Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na hisabati
na sayansi za Tiba.

Wito

HESLB
inawakumbusha waombaji wa mikopo na ruzuku wenye sifa kwa mwaka
2024/2025 ambao bado hawajapangiwa mikopo au ruzuku, kuendelea
kufuatilia taarifa za maombi yao kupitia ‘SIPA’ wakati taratibu za
uchambuzi na upangaji wa mikopo na ruzuku zikiendelea.

Imetolewa na:
BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU
Jumatano, Oktoba 09, 2024.

KUCHEKI MAJINA HESLB, CLICK HERE!

logoblog





JOIN US ON TELEGRAM
Get Notifications Faster by:

5 New Various Jobs at SHDEPHA+ Tanzania October 2024

Marketing Officer at Saacta Enterprises Company Limited