in , , , , , , , ,

HESLB Majina Ya Waliopata Mkopo Awamu Ya Kwanza 2024/25

HESLB Majina Ya Mkopo Awamu Ya Kwanza 2024/2025 Academic Year
HESLB

HESLB, Majina Ya Waliopata Mkopo Awamu Ya Kwanza 2024/2025 Academic
Year, Majina Ya Waliopata Mkopo 2024/2025, Majina Ya Waliopata Mkopo
Awamu Ya Kwanza 2024/2025, Majina Ya Waliopata Mkopo Awamu Ya Kwanza
2024, Waliopata Mkopo Awamu Ya Kwanza 2024/2025, Waliopata Mkopo Awamu Ya Kwanza 2024, Majina ya Mkopo Awamu Ya Kwanza 2024/2025, Wanuafaika wa Mkopo HESLB 2024/2025.

ORODHA YA KWANZA YA WANUFAIKA 2024/2025 YATANGAZWA

HESLB Majina Ya Mkopo Awamu Ya Kwanza 2024/2025 Academic Year

Ni awamu ya kwanza yenye wanafunzi 21,509

Mikopo yao ina thamani ya TZS 70.78 bilioni

Bodi
ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) leo Jumamosi (Septemba
28, 2024) imeanza kutangaza orodha ya wanafunzi wenye sifa waliopangiwa
mikopo kwa ajili ya mwaka wa masomo 2024/2025. Awamu hii ya kwanza
inajumuisha wanafunzi wa mwaka wa kwanza waliopangiwa mikopo ya Shahada
ya awali, Shule ya Sheria kwa Vitendo na Shahada ya Uzamili.

Wanafunzi kupata taarifa kupitia SIPA

Mkurugenzi
Mtendaji wa HESLB Dkt. Bill Kiwia amesema wanafunzi wote walioomba
mikopo kwa mwaka 2024/2025 wanaweza kupata taarifa za kina kuhusu mikopo
yao kupitia akaunti walizotumia kuombea mikopo maarufu kama ‘SIPA’ –
Student’s Individual Permanent Account.

“Leo tumeanza kutoa
taarifa za mikopo kwa makundi yote, waliopangiwa mikopo, wapo ambao bado
tunaendelea kufanyia kazi maombi yao
kila mwombaji anapata taarifa yake kwenye akaunti ile ile aliyotumia
kuombea mkopo, huhitaji kufika ofisi za HESLB”, amesema Dkt. Kiwia na
kuongeza kuwa upangaji wa mikopo kwa wanafunzi wa stashahada na shahada
ya Uzamivu unaendelea.

Dkt. Kiwia amesema HESLB imeanza kuandaa
malipo ya wanafunzi wapya na wanaoendelea na masomo ambao ni wanufaika
wa mikopo na kusema lengo ni kuhakikisha fedha zinafika vyuoni kwa
wakati.

245,799 kunufaika na mikopo 2024/2025

“Mwaka
huu, Serikali imetenga TZS 787 bilioni kwa ajili ya jumla ya wanafunzi
245,799 wakiwemo zaidi ya wanafunzi 88,000 wa mwaka wa kwanza
waliotengewa TZS 284.8 bilioni,’ amesema Dkt. Kiwia na kuongeza kuwa
bajeti ya mwaka 2024/2025 imeongezeka kwa TZS 38 bilioni sawa na
asilimia 5.1 ikilinganishwa na bajeti ya 2023/2024 iliyokuwa TZS 749.4
bilioni. Mwaka huu pia kiwango cha chini cha mkopo kwa mnufaika mmoja
mmoja kimepanda hadi TZS 3.0 milioni kutoka TZS 2.7 milioni[ME1] mwaka uliopita wa 2023/2024.
Read Also:

Wito: Vyuo kuwasilisha matokeo ya mitihani

Kuhusu
wajibu wa vyuo, Dkt. Kiwia amevikumbusha vyuo ambavyo havijawasilisha
matokeo ya mitihani ya wanafunzi-wanufaika wanaoendelea na masomo,
kuwasilisha ili kuiwezesha HESLB kuandaa malipo kwa wakati.

“Kuna
vyuo vichache, ambavyo bado havijawasilisha matokeo, tumewakumbusha na
tunasisitiza waharakishe kuwasilisha matokeo ili tukamilishe malipo ya
wanafunzi waliofaulu kuendelea na masomo,” amesema Dkt. Kiwia.

Kuhusu
kutangazwa kwa orodha ya Awamu ya Pili Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB
amesema kuwa awamu ya pili ya orodha ya wanafunzi waliopangiwa mikopo
kwa mwaka 2024/2025 itatangazwa wiki ijayo

KUCHEKI MAJINA HESLB, CLICK HERE!

logoblog





JOIN US ON TELEGRAM
Get Notifications Faster by:

Sponsor Donor Support Associate I at Compassion International Tanzania

Prepaid Acquisition Manager at Airtel Tanzania Plc